Watu wasiojulikana
UTEKAJI TANZANIA SEHEMU YA 1: Liwali Naandika kwa Taifa, nchi niliyozaliwa, Kwa wote wenye nyadhifa, wajonao wana pawa, Wanasiasa kwa sifa, wachungaji na watawa, Tanzania yetu moja, sioni wetu umoja. Nianze kwako Liwali, uitwaye wa wanyonge, Wazi kemea maasi, nchi yetu tuijenge, Tutoe hofu na wasi, kutekwa tekwa wanyonge, Tanzania yetu moja, sioni wetu umoja. Hatua dhati chukua, usalama kuhakiki, Ni wengi walopotea, siamini eti kiki, Ndugu myoyo waumia, machozi hayakauki, Tanzania yetu moja, sioni wetu umoja. Kuwajua twatamani, watu wasojulikana, Watujuze waniwani, siri waliyoibana, Ni wapi aliko Beni,Pole pole na wengine Tanzania yetu moja, sioni wetu umoja. Dr smile 🩺
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
