UTU ULOPOTEA
hamjambo lakini, natumai m wazima ila niruhusini, niwaambieni kwa kina maana mtu ni utu, sio rangi na maumbile unyama tulo nawo, umetoka na wapi kuku tumekua, wenzetu kufa kawaida twaamini tu ni mazishi, na maisha kusonga kila mmoja ana haki, ya kuishi zaidi uhai Mola kampa, mwache Yeye achukue kwa aliye na akili, kifo chafaidi nini ila siku hizi twawaza, mambo ya kuuwana utu wetu jamani, alouiba ni nani mali inayo ng'ang'aniwa, haitoleta amani atabariki jasho letu, ameahidi Rabana mbona kubali kulipwa, uangamize uhai si uanzishe jambo nzuri, Mola abariki uvivu watumaliza, ulafi wa hela za haraka ubinafsi umetawala, maskini azidiwa bwenyenye atajirika, zaidi huu ulimwengu mali hizo hamtazipenda, Mola amekataa taugua vibaya, muziache duniani tamati nimefika, ila tusomeni jambo humu hatukuleta kitu, na hivyo tutarudi alotujalia Mola, tutumie kwa usawa kila mmoja ni muhimu, hamna mtu nusu Maajah Poetry
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
