ujasiri wa matumaini
Ninazungumza kwa ujasiri, sauti yangu haina uoga, Usione kama najigamba, bali kama taa katika giza nang’aa. Maisha yalinitupa mavumbini, ila matumaini nikajipa, Sasa naangaza kama nyota, si kwa kujivuna bali kuhimiza. Ninajazwa na ujasiri, nikisonga mbele bila kusita, Kwa hivyo usinione fahari, ukadhani nimejisahau. Najivunia safari yangu, kwa unyenyekevu wa moyo, Kwa kuwa kila hatua ni Maulana anayenivusha. Leo nahimiza wanyonge, kwamba kufaulu kunawezekana, Jenga moyo wa matumaini, wala si wa kujitenga. Kwa Mola ukimtegemea, mafanikio utayapata, Kwa kuwa kila hatua ni ushindi wa bidii na matumaini.
Ad
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
Shop Now →
