UCHUNGU WA JUNI
huzuni mwingi moyoni, heri yule haoni asubuhi na jioni, kumbukumbu kichwani wapendwa hawaonani, damu yao imo chini imetoweka amani, wenzangu tuhurumiane nikikumbuka Juni, damu itafukaa tarehe ishirini na tano, yahuzunisha dunia haki imepotea, sijulikane iliko kama ukweli tuambiwe, imeenda likizo wazazi wataabika, akilini na moyoni wana wao wapendwa, sasa hawaonani damu yao iliyo chini, wakiulizwa ni nani? Rabana awafariji, amani yao wapate tunalia kuuliwa, ila pia tunakosa mbona kubali kulipwa, uendeshe maafa mbona tusiwe na umoja, haki tetea pamoja mbona kubali maafa, kwa ajili ya hela cha kujivunia ni nini, wakati insani walia biashara zafilisika, uchumi unazorota ushuru muitakayo, tatoka wapi jamani biashara zikifungwa, twaelekea na wapi? Maajah Poetry
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
