UBAVU WANGU
Ewe ubavu wangu sehemu ya mwili wangu Uwepo wako taa yangu yani gizani sina taabu Natazama mwisho wa upeo wangu hakuna kama wewe ubavu wangu napambana napigana ili ule mkewangu nakuamini ubavuwangu nitunzie wanangu. Sauti ya bahari ni kuu sana na huvutia fukwe ila Sauti yako kwangu huisha wangu upweke nizawadi gani nikupe marikia wangu nikitazama sioni cha kukufaa ubavu wangu au nikufanye maraika mkewangu mbinguni tukaishi kwa Mungu. Yule nilimpenda jagwani alinitupa kiu kilinishika machozi yalinivuja Ubavu wangu ukaniokota upendo ukanivisha baridi ikanipita machozi ukanifuta Raha ukanipa sina cha kujivuna ila wewe ubavu wangu Nikufananishe na nini rohoyangu kwani dhahabu huyeyuka mitoni fedha hupukutika kama majani mtini mali hupotea kama shiringi baharini lakini wewe umeganda moyoni mwangu mfano wa barafu zizizopo mwisho wa dunia
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
