PENZI VAMPIRI
wenzangu nastaajabu, vampiri upendo umekuwa wasichana sijaribu, kile kinacho wauwa haya twende taratibu, maana ni vyema kujua wachana na mahabubu, wataja kukuuwa huzuni imetanda, pembeni zote za dunia haswa humo vilabuni, pia nyumba za kukodisha kama kuku wanachinjwa, penzi geuka vampiri wachana na mahabubu, wataja kukuuwa pole pole lianza, ukadhani ni mchezo kuonana mkaanza, mpaka ndani ya ndoto mapenzi yalokuwa asali, yanageuka vampiri wachana na mahabubu, wataja kukuuwa uvivu tulonawo, chanzo cha hili vampiri wa kodi wa vipodozi, na pia wa sherehe shilingi yako muhimu, maana ni bidii yako wachana na mahabubu, wataja kukuuwa mate machungu mtameza, maana ukweli wauma nimechoka kutazama, mapenzi yalokinzana sitokata tamaa, vipusa kuwakanya wachana na mahabubu, wataja kukuuwa tamati ninakoma, mapenzi ya walokomaa tulowandogo jithibiti, tukomeshe vampiri maana sana nauliza, ni mapenzi au vampiri? wachana na mahabubu, wataja kukuuwa Maajah Poetry
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
