NAYE KUMBUKA
sura yako mtaratibu,mwandishi wa sanaa kusahau najaribu, ila nakumbuka sana maneno yako tabibu, nadai yangu yaiponya kusahau najaribu, ila nakumbuka sana alonifanya silali,chemia kati yetu sidhani bila hata kujali,na hatari mie sidhani yupi bado akilini,na kusahau sidhani kusahau mejaribu,ila nakumbuka sana maneno yake asali, yanasa zangu fikra midomo yake chingamu,isiyo isha utamu ulimwengu huu yanitoa,nadhani fantasia kusahau mejaribu,ila nakumbuka sana ndevu zake laini,vyema zimetunzwa wosia wake amini,mengi taja funzwa na pia ni mwamini,wake mwenyezi Rabana kusahau mejaribu, ila nakumbuka sana siwezi danganywa na wale,kando niende ilanifuate na yule,moyo atulizaye kama furaha na waidha,ndiye anipaye kusahau mejaribu, ila nakumbuka sana Maajah Poetry
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
