MWANAUME PIA HULIA NY: SHEILA
Mwanaume pia hulia, ila kwa kimya, Kimya chake ni kilio kisicho na sauti. Msongo wa mawazo humlemea bila hila, Maumivu moyoni— mia kwa mia—huwa machungu ya kweli. Kulia si kosa, wala si dhambi, hata simba hulia, Tusimwite dhaifu anapolilia na kuhema. Tumpeni nafasi, aweze kuelezea Yaliyomsonga rohoni, bila aibu wala lawama. Jamii humfundisha avumilie, abebe bila kulalama, Lakini dhoruba za fikra, humchana kwa makali. Leo mpe mwanaume nafasi ya kuongea na kujieleza, Maana hata ngome huhitaji ukarabati wa ndani. Mwanaume shujaa ni yule anayejua Kuomba msaada pale anapohitaji Kuipa afya ya kiakili kipaumbele Tujenge jamii yenye nguvu na matumaini
Ad
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
Shop Now →
