MWANAMKE HODARI
leo siku njema, nakumbuka wangu shujaa nashukuru Karima, salama tumefikia mempata humu Tala, salamu zangu pokea mwanamke hodari, mwalimu wangu wa kemia namuomba Rabana, neema alokujalia anijalie pia mimi, heri niwe naivutia nijitume usiku kucha, niwe nisiwe na afya mwanamke hodari,mwalimu wangu wa kemia hasira yake kilio, furaha yake sherehe ni mkali hakika,ila mpole ukitaka vituko mevumilia, makosa menikosoa mwanamke hodari, mwalimu wangu wa kemia tatizo likitokea, tayari una suluhu akili zako za ncha, wajua yote ya sayansi jina lako majazi, kweli Bi.Muema jamani mwanamke hodari, mwalimu wangu wa kemia Tamati nimefika, naomba niruhusu wosia wako hakika, mambo tukiyadurusu sinalo la kusema,nakuombea baraka mwanamke hodari, mwalimu wangu wa kemia Maajah Poetry
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
