MWALIMU BI.MAKAU
leo siku yetu,tuyatoe ya moyo wetu shukrani mwalimu,kwa kazi yako bora bi.Makau malkia,wetu wa hisabati twashukuru Karima,wewe kukupata kwa mafunzo yako bora,daima human kifani kwa zako tele busara,na mwongozo maishani wewe ni kinara,nuru yetu maishani wewe ni zawadi,mwalimu bi.Makau awe mkali au mpole,sana twajivunia imekuwa ndefu safari,tena yenye mengi kuzuri au kubaya,yote hayo ni mengi kwaheri bi.Makau,Rabana akubariki tukija watupokea,karibu ofisini unatupa na furaha,mawazo yatutoka tukikwama wakwamua,vikwazo watuvusha kwaheri bi.Makau,Rabana akubariki imara twafurahi,masomo Mbusyani serikali katupa,zawadi ya thamani wewe shujaa wetu,hatuna wa mbali kwaheri bi.Makau,Rabana akubariki hakuna cha kukulipa,wala hakionekani chochote tunachokupa,hakifiki thamani sala twaiweka hapa, akubariki Manani maadili ulotupa,tutilie maanani Maajah Poetry
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
