MWALIMU BI. MUNYAO
Nampenda nampenda, niulizeni ni nani Meumbwa kaumbika, maridadi jamani Jina lake lapendeza, tabia pia ajali Zangu salamu pokea, mwalimu Bi.Munyao Kushoto pia kulia, hayupo wako kifani Naona nikija lia, ila yale ya furaha Gizani menitoa, mwangazani menileta Zangu salamu pokea, mwalimu Bi.Munyao Maneno yako tamu, tena yenye busara Umejawa tabasamu, huzuni kwako ni nadra Siku nenda siku rudi, amani menifanyia Zangu salamu pokea, mwalimu Bi.Munyao Presha mingi mawazo, Kathambi sina tena Waidha lako ninalo, daima niishipo Niwe nisiwe na afya, bado nitakumbatia Zangu salamu pokea, mwalimu Bi.Munyao Nimejawa na furaha, shukrani tele teke U rafiki mwema, tena yule wa karibu Nakuombea na mema, akubariki Rabana Zangu salamu pokea, mwalimu Bi.Munyao Tamati nimefika, naomba niruhusu Wosia wako hakika, mambo nikiyadurusu Sinalo la kusema, nakuombea baraka Zangu salamu pokea, mwalimu Bi.Munyao -Ibmahtak Htur
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
