mapenzi ni kama njugu
Kama mapenzi ni hisia, Mbona kupuuzwa Ulieleta roho yako mtaani, Kwa mtu alikuwa na roho ya barafu, Ukamwaga feelings kama maji ya mtungi, Na yeye akaswipe left kama ni story ya last week. Nilikupenda na roho safi, Kama vile Gikosh hupenda wateja, Lakini ulipotea, Kama stima Eastlando jioni ya Friday. Nilikuwa nachora ndoto zetu kwa kuta za mind yangu, Ukazifuta kama graffiti kwa wall ya chief, Na bado najiuliza – mbona mapenzi ni swali bila jibu? Ulinijaza hope kama mat za Kayole kwa peak hours, Nikajua tuko safari moja, Kumbe ulikuwa una-drop off stage moja kabla yangu, Na ukaniwacha nikishika feelings kama nguo za Second Hand. Ulinijua nikikam kutoka job nikiwa na jasho ya hustler, But still nilikuletea smile, Na wewe ukanipea blue ticks, Zenye zinachoma zaidi ya mchele bila chumvi. Mapenzi ni kama njugu, Ukipasua moja, unapata mawili; Hapo ndipo nilijua, Si kila anayekulenga anakutaka – wengine wanatafuta tu mtu wa kuslide naye boredom. Saa hii nimeshika hamsini ya life, Feelings zimegeuka kuwa streetwise, Situpi tena roho kwa mtu ambaye hawezi beba ata secrets zake mwenyewe. Najiuliza, kama mapenzi ni furaha, Mbona kupuuzwa ni maumivu ya deep kama ngumi ya life? Sijui, mtaa ulinifundisha kupenda vibaya
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
