maisha
Maisha haya maisha, yana uzuri na ugumu, Magumu nayo yataisha, katu usijilaumu. Tamaa zitakukatisha, usiyape hata umuhimu, Nakupenda rafiki, jitunze! Mapenzi ni hatari, waja walilileta, Nayo hayana mshauri, akiingia ubaya ataleta. Hoja zake hatari, chamtema kuni utapata. Nakupenda rafiki, jitunze! Maisha yana mapigo, nayo yanaliza, Yatakupa na mizigo, mapenzi ukiyaingiza. Utapata na kipigo, maisha ukiigiza. Nakupenda rafiki, jitunze! Nakuletea na tumaini, nye maisha lipokee, Mapenzi nako niamini, raha ujizolee. Sikate tamaa maishani, amini yatakwisha, Nakupenda rafiki, jitunze!
Ad
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
Shop Now →
