JUKUMU
waungwana sikizeni, muifikisheni habari kwa upole welezeni, ata wale wa mbali amezaliwa mwokozi, mfariji ule wa kweli tuungane kwa pamoja, tuje mkaribisha aliuwacha ufalme, aje kwa ajili yetu kwa dunia tusizame, kusherehekea kivyetu muhimu tukumbuke, jukumu lake kubwa kuja kutuokoa, kuondoa dhambi zetu tuli tuje tulia, kusherehekea kwa imani hakuja ili tulewe, alija tuokolewe nyota yake imeshang'aa, pia sisi tunang'aa ni siku kubwa jamani, kwa wote tulio wake maisha ya taabu, na nyingi dharubu mengi tuliyoyajaribu, naye yalifaulu ni rafiki wa karibu, yaani kwetu ni dhahabu mauwa ya dhamani, tumpeni yaloheri habari tusambazeni, tuwaambieni kwa kina pia humo vijijini, muhimu kukumbuka sababu ya kuzaliwa, kubwa ni kuokolewa tuwekeni sherehe, ziheshimio jukumu sasa twatarajia heri, na furaha isokwisha amezaliwa mwokozi, giza twaitetemesha nuru yake haina kifani, ndiyo tumeshikilia ulimwenguni halisi, na pia wa kiroho tamati nimefika, yatosha niloyasema nyote nawatakia, sherehe ilotukuka ijawe na furaha, na neema kwa wingi yote hayo kulingana, na mapenzi ya Mola Maajah Poetry
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
