HESHIMA MUHIMU ZAIDI
ndugu zangu sikieni, haya nayo waambia msije kapuuzeni, mwisho mkaja jutia piga teke kiburi, maadili kumbatia heshima muhimu sana, zaidi kujiheshimu sipeane ovyo ovyo, utu wako jamani pesa hizo uzionazo, waeza kosa faidi ubikra kisha potea, kamwe haurudi tena sijitie najisi, anasa achana nayo meumbwa kaumbika, ila maadili hakuna anasa imekunasa, mwelekeo hauna kwani hujipendi,utamani maisha mema shinikizo rika epuka,maadili kumbatia mjini vijijini,tatizo lilo hilo maadili kutozingatiwa,yamefanywa ujadi wazazi wataabika,akilini na moyoni waomba usiku kucha,wanao wajisetiri vifo vingi vya mapema,vyatokana na vileo anasa sio ustaarabu,wajichimbia kiburi siutamani baadaye,maishani uhigwe mfano sio mfano wowote,ila mfano mwema Maajah Poetry
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
