HESHIMA MUHIMU
ndugu zangu sikieni, haya nayo waambia msije kapuuzeni, mwisho mkaja jutia piga teke kiburi, maadili kumbatia heshima muhimu sana, zaidi kujiheshimu meumbwa kaumbika, ila maadili hauna anasa imekunasa, mwelekeo hauna pesa hizo uzionazo, waweza kosa faidi heshima muhimu sana, zaidi kujiheshimu twalalama kubakwa, ila pia twachangia washa sema wahenga, macho hayana pazia tusivyo jivika vyema, nini basi twatarajia heshima muhimu sana, zaidi kujiheshimu mjini vijijini, tatizo lilo hilo maadili kutozingatiwa, na kufanywa ujadi wazazi wataabika, akilini na moyoni waomba usiku kucha, wanao wajisetiri vifo vingi vya mapema, vyatokana na vileo anasa sio ustaarabu, wajichimbia kaburi kwani wewe hujipendi, utamani maisha mema heshima muhimu sana, zaidi kujiheshimu Maajah Poetry
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
