HALALI WANGU
natuma salamu zangu ziende kwa halali wangu tulizo la roho yangu Njogu uzawadi kubwa kwangu unaenipoza machungungu yaani halua yangu, o Njogu namshukuru Manani kwa kunipa wewe mwema ulosafika moyoni mwenye wingi wa huruma umeumbika yakini mzuri kikutazama sauti yako laini o Njogu ni mgonjwa taabani, we ndio daktari wangu nimekupata mwendani, kwa uwezo wake Mungu niingiapo nyumbani, utua wangu mzima kuenda nje sitamani, kwako wewe nishazama tena uniamini, sitokuacha daima adi tuingie peponi, amina tuli nimetulia, roho yangu imepoa ewe wangu naridhia, o raha Maajah Poetry you
Ad
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
Shop Now →
