ELIMU NI BARAKA
elimu ni baraka, iletayo faraja ila kama tambara, lisilo wake ubora ajira imetoweka, wazee wamekatalia elimu ni baraka, acha ibakie vile mvi wanayo kichwani, ila bado wa kazini vijana wetu walosoma, njiani mefurika wavyele lijinyima, ili elimu kuwapa elimu ni baraka, acha ibakie vile madeni wana mengi, yalolipia na karo tumaini pia nyingi, wanao wafaulu ila uongozi mbaya, hayo yote umemeza elimu ni baraka, acha ibakie vile bidii wanatia, wanafunzi shuleni iwe ni sekondari, ata pia chuoni wanatenda yote hayo, ili waje faulu elimu ni baraka, acha ibakie vile suluhu kubadili, uongozi mbaya ufisadi tupiliwe, mbali sana hakika pia wastaafu, wafaao kustaafu elimu ni baraka, acha ibakie vile Maajah Poetry
Poetry Books 50% Off
Bestselling collections from top poets
